Taarifa ikufikie kwamba imepigwa marufuku kwa jinsia ya kike kuvaa nguo fupi (ki-mini) nchini Uganda na tayari Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni amesaini rasmi sheria hii.
Japokua baadhi ya Wabunge walipinga kwamba marufuku hii inaingilia uhuru wa mtu kuvaa, wabunge wengi wameunga mkono uamuzi huu.
Unaambiwa marufuku hii ambayo imelenga kuepusha vitendo vya ubakaji na ngono zembe kutokana na ushawishi unaotokana na uvaaji huu, inahusisha pia nguo nyingine fupi ambazo zinaacha sehemu kubwa ya mwili wazi kama vile kifuani.
Wanawake/Wasichana wataruhusiwa kuvaa mavazi mafupi kwenye matukio maalum tu yanayohusisha uvaaji huu kama vile michezo ambapo Waziri husika Sheria hii pia inawabana Wanamuziki wa kike ambao wamekua wakivaa nguo fupi kwenye show zao pamoja na video ambapo Waziri Lokodo amesema ‘hatutaki uhusike kufanya watu wakutamani au watamani kufanya ngono, hatutaki ushawishi chochote kwa jinsia ya kiume, kuwa na tabia njema kwa kuvaa kiheshima’
Vilevile vyombo vya habari yakiwemo Magazeti na TV, vimepigwa marufuku kuonyesha picha za watu wakipigana busu au picha zozote za Wanawake wakiwa nusu uchi.