Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amezitaka Shule zote za binafsi ndani ya Wilaya hiyo kuhakikisha zinaweka Msaidizi wa kike (Matron) kwenye kila Basi la Shule badala ya Msaidizi wa kiume (Patron) na kwamba Serikali haitoivumilia Shule yoyote itakayoshindwa kufanya hivyo.
DC Godwe ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari ndani ya Wilaya hiyo ambapo amenukuliwa akisema… “Kinondoni tumeamua kwa zile Shule zote zenye School Bus wawekwe Matrons kwenye kila Basi la Shule, lengo ni kutengeneza mazingira mazuri kwa Watoto kutopata unyanyasaji wa kijinsia, tusingependa kuona mambo yaliyotokea mwaka jana yatokee tena mwaka huu”.
View this post on Instagram