Habari ya Asubuh!….Karibu kufuatilia matangazo yetu hii leo Alhamisi 10.8.2023
Watu wasiopungua 33 wamethibitishwa kufa na wengine 18 bado hawajulikani waliko baada ya kushuhudiwa mvua kubwa mjini Beijing China.
Mji huo mkuu wa China umekumbwa na kiwango kikubwa cha mvua katika wiki za karibuni, ambacho kimeharibu pakubwa miundombinu na kusababisha mafuriko katika vitongoji vya jiji hilo na maeneo ya jirani.
Watu kadhaa wamefariki dunia katika mafuriko kaskazini mwa China, huku maafisa wa Beijing wakisema kuwa vifo au kutoweka kwa watu 147 mwezi uliopita kulisababishwa na majanga ya kimaumbile.
Taarifa zaidi kutoka Beijing China zinasema, maelfu ya watu wamebaki bila makazi baada ya nyumba zao kusombwa au kuharibiwa kabisa na mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko.
Beijing imekumbwa na rekodi ya mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni, huku mafuriko yakisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na kuharibu maelfu ya nyumba.
Maafisa wa jiji hilo wameziambia duru mbalimbali za habari kwamba, takribani nyumba 59,000 zimeporomoka kufuatia janga hilo la mafuriko huku zingine zipatazo 150,000 zikiharibiwa,hususan katika viunga vya milimani vya magharibi mwa mji mkuu Beijing.
Mafuriko hayo pia yamesababisha madhara makuubwa katika ardhi ya mazao, ambapo inaelezwa kuwa, zaidi ya ekari 37,000 zimeathiriwa. Aidha barabara nyingi katika eneo la jiji pia zimeharibiwa na kusababishwa baadhi ya madaraja kutopitika.