Tanzania na Kenya ndio nchi pekee za Afrika Mashariki ambazo zinaongoza kwa kuzungumza sana lugha ya Kiswahili tofauti na Rwanda, Burundi na Uganda.
Katika vitu ambavyo nilikua sivijui ni pamoja na hii kwamba pamoja na Wakenya kuwa mahiri kwenye kuongea Kiswahili, wanalo gazeti moja tu la Kiswahili linalotoka Nairobi liitwalo Taifa Leo huku hayo mengine yaliyobaki yakiwa ni ya Kiingereza.
Navutiwa na aina ya kiswahili chao wanachokitumia kwenye vichwa vya habari mfano hii waliyoandika ‘Nyota kutoka Afrika wenye visura tamanifu’
Naambiwa gazeti hili linafanya vizuri sana kwenye mauzo na lina rekodi ya kuuzika bila kopi kubaki, vilevile ni gazeti lenye miaka na miaka toka kuanzishwa kwake miaka ya 50.