Rais wa Jamuhuri ya Kenya Dkt William Ruto ametangaza hivi karibuni kuanza ujenzi wa barabara ambayo itatokea Mombasa mpaka Tanga bara bara ambayo wamekubaliana kama mataifa ya afrika Mashariki kwamba itasaidia kwenye kurahisisha usafiri na uwekezaji.
“Nilikua hapa juzi katika ile barabara ambayo inatoka kule kirifi ambayo itaungana na barabara hii itaenda mpaka ikaungane na ndugu zetu watanzania, Kutoka hapa ferri mpaka ifike mpakani kwetu na Tanzania na mpaka ifike kule Tanga hiyo barabara vile vile tumekubaliana kama east africans na tumekubaliana kwamba hiyo itatusaidia kurahisisha usafiri na kurahisisha uwekezaji”
Aidha Rais Ruto amesema kuwa ndani ya miaka mitatu ijayo serikali ya kenya itafanya kazi na wale wote wahusika kuhakikisha kuwa kila nyumba ndani ya ya nch ya Kenya itakua na mtungi wa Gas na kuhakikisha ya kwamba bei ya gesi inapungua kwasababu serikali itaondoa ile kodi yote ambayo imewekwa kwa mambo ya gesi.