Meneja wa shirika la Umeme nchini ( TANESCO) Mkoa Morogoro Mhandisi Fadhiri Chilombe amesema kituo Cha Kupokea,kupooza , kusambaza umeme Cha msamvu kimepata hitilafu na kusababisha Maeneo mbalimbali kukosekana kwa huduma hiyo kwa msaa kadhaa.
Mhandisi Chilombe amesema hayo baada ya kutembelea kituo hicho ambapo amesema kituo hicho kilipata hitilafu siku ya Jana septemba 14 ambapo tayari mafundi wanaendelea na matengenezo.
Amesema baaada ya kutokea changamoto hiyo shirika limeendelea na mikakati ya kurejesha huduma katika Hali ya kawaida kwa kuedelea na matengenezo.
Chilombe amesema maeneo yaliyoathirika zaidi baada ya kutokea hitilafu katika kituo Cha Msamvu ni Maeneo ya Morogoro mjini,Bwawa la Mwalimu Nyerere,Mvomero , Morogoro vijijini .
Aidha Mhandisi Chilombe amesema hitilafu iliyotokea ni ya kawaida Katia masuala ya kiufundi na haihusiani na changamoto zilizokua zinatokea siku za nyuma katika kituo hicho.
Ikumbukwe kua kituo hicho kimekua kikipata hitalafu Mara kwa Mara ambapo miezi kadhaa iliyopita kimeugua Mara mbili mfululizo na kusababisha umeme kukatika Maeneo mengi