Katika Hali isiyo ya kawaida Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mikumi Mpya mwenye umri wa miaka (11) Aqram Isihaka pamoja na mama yake mzazi Farida Habibu wameshindwa kujizuia na kuanza kulia mbele ya hadhara baada ya mtoto huyo kuwasili kutoka jijini Dodoma alikokuwa anashiriki mashindano ya wabunifu kitaifa na kuibuka mshinda nafasi ya kwanza nchini.
Mwanafunzi huyo alibuni Kamusi ya kutumia umeme ambayo inauwezo wa kutafsiri michoro ya wanyama na vitu mbalmbali.
Pia amebuni kifaaa kingine maalumu kwa watu wenye Ulemavu wa kuona na kusikia ambayo inatumia umeme kuwaka taa na kupiga kelele .