Benki Kuu ya Tanzania ‘BoT’ imetangaza mabadiliko yatakayohusisha maduka ya kuuza na kununua fedha za kigeni “Bureau de Change” ambapo kabla ya mabadiliko haya kulikuwa na kanuni za kusimamia maduka hayo yanayojihusisha na biashara ya kuuza na kununua fedha za kigeni.
Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Kanuti Mosha kutoka Kurugenzi na Usimamizi wa Mabenki na Taasisi za Fedha anasema:>>>”Tangazo la Serikali lilitolewa June 2, 2017 kufanya mabadiliko kidogo katika kanuni za 2015 ambapo mitaji imeongezeka. Kwa Daraja A mtaji umeongezeka kutoka milioni 100 na sasa utakuwa milioni 300.
“Daraja B mtaji umeongezeka kutoka milioni 250 mpaka bilioni Moja na amana imeongezeka kutoka dola 50,000 kufikia dola 100,000. Mabadiliko haya tulitoa waraka kuwajulisha wananchi na wamiliki wote wa maduka ya fedha kwamba watahitaji kuhakikisha kwamba wanatimiza matakwa ya mabadiliko haya ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu June 2 mpaka September 1.” – Kanuti Mosha.
Ulipofikia urejeshwaji wa Mikopo ya Elimu ya Juu!!!