Rais Barack Obama wa Marekani amekutana na Papa Francis wa kanisa katoliki Alhamis ya March 27 2014 katika mji wa Vatican ambako Papa anakaa, ambapo ameitumia nafasi hiyo kufanya mazungumzo juu ya uongozi wa kikanisa pamoja na uongozi wa Marekani miaka kadhaa ijayo.
Lengo kubwa la mkutano huu ni kuzungumzia zaidi juu ya vitu wanavyokubaliana na wanavyotofautiana wakiwa pia na nia ya kushirikiana katika kupinga umaskini na kupinga ukuaji wa kukosekana kwa usawa.
Mambo mengine ya kujadiliwa yalikua ni na ndoa za jinsia moja na utoaji mimba kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani.
Kwenye mahojiano na gazeti la Italia, Rais Obama amezungumzia wasiwasi wa Papa kuhusu usawa wa mapato akisema “hii si habari ya uchumi tu, bali pia ni ya maadili, nadhani Papa alikua akizungumzia hatari ya kwamba kila siku tunaizoea hali hii ya kutokua na usawa wa mapato na kuikubali kama ni kitu cha kawaida lakini hatuwezi”
Obama amesema anapenda ujasiri wa Pope wakati anazungumzia uchumi na mambo mengine ya kijamii na kukaririwa akisema ‘haimaanishi kwamba tunakubaliana na kila kitu lakini sauti ya Papa ni sauti ambayo dunia nzima inatakiwa kuisikia, anatupa changamoto na kutufanya tukumbuke wenzetu hasa walio maskini ambao wameathiriwa na maamuzi ya uchumi tunayotengeza sisi”
Hii video hapa chini inamuonyesha Obama akiwa anawasili kwa Papa na jinsi alivyopokelewa.
[youtube youtubeurl=”G0u34dZ4yM4″ ][/youtube]
[youtube youtubeurl=”E3ywf8Hhiu4″ ][/youtube]
[youtube youtubeurl=”cHIwjBcp0io” ][/youtube]