Rais Magufuli leo August 3, 2017 ameanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga ambako amesema Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya watu waliouziwa mashamba makubwa Mkoani Tanga na kuyatelekeza ambapo mpaka sasa hati miliki za ardhi 5 zenye zaidi ya ekari 14,000 zimefutwa.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Mkata, Komkonga, Kabuku, Michungwani, Hale, Muheza na Pongwe katika Wilaya za Handeni, Muheza na Tanga Rais Magufuli amefafanua kuwa Mkoa wa Tanga una mashamba 72 yaliyouzwa kwa watu mbalimbali ambapo hatua za kunyang’anya mashamba yaliyotelekezwa zimeanza kuchukuliwa kwa mashamba 12 na tayari mashamba 5 ambayo hati zake zimeshafutwa, utaratibu unaendelea kuwagawia wananchi na wawekezaji watakaokuwa tayari kuyaendeleza kama ilivyokusudiwa.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza shamba la ekari 50 lililopo katika kijiji cha Kabuku ambalo lililotolewa na wananchi kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa lengo la kujenga kiwanda miaka 7 iliyopita, lirejeshwe kwa wananchi na ametaka JKT ijenge kiwanda hicho katika eneo lake jingine lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 9,000.
Aidha, Rais Magufuli ametoa siku 15 kufanyika kwa uchunguzi wa fedha Tsh. Milioni 500 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kituo cha afya cha Mkata, kufuatia kuwepo kwa taarifa za ufujaji wa fedha hizo na kuongeza kuwa Serikali itapeleka Tsh. Milioni 800 kwa ajili ya kuendeleza kituo hicho baada ya hatua stahiki kuchukuliwa.
>>>”Siku 15 tuwe tumepata jibu ili fedha nyingine Shilingi Milioni 800 zije, kama huyo Mkandarasi hafai afukuzwe, kama kuna mtu hafai aondolewe, tuanze na ukurasa mpya, na ningeomba Mkuu wa Wilaya ulifuatilie hili ili asiponyoke mtu yeyote, na wewe una Mamlaka yote.” – Rais Magufuli.
ULIPITWA? Agizo Rais Magufuli amelitoa kwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS…tazama kwenye video hii!!
“Matatizo yaliyo kwenye uwezo wa Kiongozi na hakuyatatua, nalala mbele na huyo Kiongozi” – JPM