Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewatoa hofu Wananchi kuwa hadi sasa Tanzania haina mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya corona huku akiwataka Wananchi waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu, pia waepuke kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa na Serikali.
“March 13, asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) walipokelewa wasafiri sita wakitokea Kenya, wawili ni Raia wa Denmark na wawili ni wa Norway (Wanawake watano na Mwanaume mmoja) baada ya ukaguzi mmoja alikutwa na homa, kikohozi na mwili kuchoka” – Waziri Ummy
“Wasafiri wote sita walitengwa katika Hospitali ya Mawenzi na kuchukuliwa sampuli zao ambazo zilipelekwa maabara DSM, uchunguzi umebaini wote hawana maambukizi, msafiri aliekutwa na joto kali amebainika kuwa na mafua ya kawaida, wote wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao”-Waziri Ummy