Msichana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Kaskazini mwa Nigeria huko Kano amekiri kumuua mwanaume alimuoa kilazima kutokana na shinikizo la wazazi uamuzi ambao hakuridhishwa nao kabisa.
Wasilu Umar amemuua Mume wake ambae alikua na umri mara mbili ya umri wake kwa kumuwekea sumu ya panya katika chakula chake kitendo kilichosababisha watu wengine watatu kufariki na 10 kukimbizwa hospitali baada ya kuhusika kwenye hicho chakula.
Baba wa mtoto huyo alimlazimisha kuolewa na mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 35 ambapo harusi yao ilifanyika wiki iliyopita hukohuko kaskazini mwa Nigeria ambako ni maarufu kwa kuoza watoto wakiwa na umri mdogo.
Polisi wamekua wakijaribu kusitisha ndoa hizo za kulazimishwa ambapo baba wa Mtoto anaweza kushtakiwa juu ya hilo kosa ila bado hivyo vitendo vinaendelea.