Dar es salaam ndio mji unaoongoza kwa foleni ya magari Tanzania ambapo wakati mwingine unaweza kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu mpaka anaesafiri kwa ndege ya Fastjet kutoka Dar mpaka Zambia (dakika 135) au Kilimanjaro mpaka Dar es salaam (dakika 60) akawahi kufika kabla yako.
Unaambiwa kati ya mwaka 2008 mpaka 2013 kuna jumla ya magari madogo laki mbili na elfu ishirini na sita (226,806) yaliingizwa nchini Tanzania ambapo asilimi 70 yanatumika Dar es salaam.
Kingine cha kufahamu ni kwamba kwa mwezi, Watanzania hununua magari madogo yanayokadiriwa kuwa zaidi ya 4500 ambapo mengi kati ya hayo hutumika ndani ya jiji la Dar es salaam kwa mujibu wa @BBC_Habanahaba
Magari mengi yanayotumiwa ni kutoka kampuni ya Toyota Japan kama vile Mark X na aina nyingine mbalimbali huku Japan ikiwa ni nchi ambayo magari inayotengeneza yamekua yakipata soko kubwa sana kwenye nchi mbalimbali za Afrika kutokana na kuweza kuhimili mazingira magumu ya nchi zenyewe.