Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Magazeti yote ya Tanzania leo Nov 19 2016 na habari zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho pic.twitter.com/uKDidmKyuI
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
#MTANZANIA RC Makonda aanika ushahidi mwingine wa Shisha Kamanda Sirro kutoa ya moyoni wakati DCI Boaz akisema wameanza uchunguzi wa tuhuma pic.twitter.com/wLftmG7Ggs
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
SASA ni dhahiri kwamba sakata la kilevi cha shisha limewavuruga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro, baada ya kila mmoja kutoa utetezi wake wa namna operesheni za kukidhibiti inavyofanyika.
Hali ya kuvurugana huko imetokea baada ya Makonda kumtuhumu Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha uboreshaji huduma za umeme, iliyofanyika Dar es Salaam juzi, mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwamba huenda wanapokea rushwa ya Sh milioni 50 kutoka kwa kikundi cha wafanyabiashara 10 (kila mmoja aliahidi kutoa Sh milioni tano) wa kilevi hicho waliomshauri azichukue yeye kila mwisho wa mwezi ili waendelee kufanya biashara hiyo, lakini alikataa kwa kile alichodai kuwa walikuwa ni mawakala wa shetani.
Makonda aliendelea kutoa tuhuma hizo kwamba, pengine kutokana na rushwa hiyo ndiyo maana Sirro na Kaganda wanalegalega kuwakamata wafanyabiashara hao waliomfuata ofisini kwake, licha ya kuwaagiza kufanya hivyo.
Licha ya Makonda kutoa tuhuma hizo, lakini Majaliwa alimtaka kufuatilia maagizo aliyowapa kina Sirro na asipofanya hivyo atamwajibisha kwa kushindwa kusimamia maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu serikalini, ikiwamo kupiga marufuku biashara ya shisha jijini Dar es Salaam.
Kutokana na tuhuma za kina Sirro kuibua mjadala, Makonda aliendelea kuzizungumzia katika kipindi cha Power Break Fast, kilichorushwa jana na Kituo cha Redio cha Clouds FM, kwa lengo la kutoa ufafanuzi zaidi na alisema anashangaa kuona vyombo vya habari vikizungumzia zaidi kauli yake badala ya kuelimisha madhara ya shisha.
#NIPASHE Mahakama Kuu kanda ya Mwanza jana imempa ushindi Ester Bulaya kuwa Mbunge halali wa Bunda na kutupilia mbali kesi ya Stephen Wasira pic.twitter.com/Xs02a9UE8k
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#UHURU Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dr. Leonard Maboko amesema pamoja na juhudi za Serikali, Virusi vya UKIMWI bado ni tatizo hapa nchini pic.twitter.com/jxROSqzjFz
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#UHURU Miamba ya Soka nchini England Man U na Arsenal leo inashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini humo pic.twitter.com/DYTbFjIvbo
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#MWANANCHI Waziri William Lukuvi amesema ameshakabidhi polisi majina ya watu 30 wanaodaiwa kuwa ni matapeli wa Ardhi ili washaghulikiwe pic.twitter.com/ZFWz04EpQ1
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#TanzaniaDAIMA Jeshi la Polisi Tanzania limetoa siku 30 kwa wananchi wanaomiliki Silaha kuzihakiki huku ikitoa onyo kwa watakapuuzia agizo pic.twitter.com/s1tMONZmeZ
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#UHURU Serikali imewahakikishia wananchi watakaopitiwa na mradi wa ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa Bagamoyo mkoani Pwani watalipwa fidia pic.twitter.com/DYyMfmqDf0
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#UHURU Nyota mpya wa Azam FC Samuel Afful ameweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa moto kuelekea michuano mbalimbali itakayoanza kushiriki pic.twitter.com/As87tRANYA
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#UHURU Msanii mkongwe wa BongoFlava TID amesema kuwa muziki huo unapoteza ladha kutokana na wasanii wengi kuiga wasanii wa nje ya nchi pic.twitter.com/2RErmllc1v
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
#JamboLEO Wadau wa Elimu wameshauri Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuweka utaratibu utakaosaidia kuwapata wadaiwa na sio kwenda mahakamani pic.twitter.com/uaG1kTMkxC
— millardayo (@millardayo) November 19, 2016
VIDEO: Alice Tupa anazo story zote kubwa kwenye Magazeti ya leo November 19, 2016. Unaweza kutazama video hii hapa chini.