Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu leo July 13, 2017 imeahirisha kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa sababu ya matatizo ya kiafya yanayomkabili.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameeleza baada ya baada ya Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kueleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa ambapo hata hivyo, Wakili wa Masogane, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe.
Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi July 25, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Video Queen, Agnes G.'Masogange' imeahirishwa hadi July 25, mtuhumiwa ana matatizo ya kiafya. pic.twitter.com/8VvxH5stZD
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
EXCLUSIVE: Majibu ya Tundu Lissu kuhusu kumfuta uanachana Waziri Mwakyembe!!!