Utafiti mpya umebaini kuwa mwewe wamekuwa wakijizuia kuingia nchini Ureno kufuata chakula, na badala yake hupendelea Hispania kutokana na sheria kali zinazozuia kusambaa kwa ugonjwa wa kichaa cha ngombe nchini Ureno.
Watafiti kutoka nchini Ureno na Hispania waliwawekea alama mwewe 72 kwa miaka mitatu na kugundua kuwa ni 13 tu waliongia nchini Ureno kwa kipindi hicho.
Eneko Arrondo kutoka kundi la watafiti la Donana Biological Station, anasema sheria kali za Ureno zinazozuia kusambaa kwa ugonjwa wa kichaa cha ng’ombe, zinawataka wakulima kuondoa mizoga yote mashambani. Hii inamaana kuwa ndege hao hawapati fursa ya kula mizoga hao.
Hispania ilitumia nafasi hiyo kuyapa mabaraza kuamua ikiwa wangeiacha mizoga hiyo mashambani kwa kuwa nchi hiyo ni nyumbani kwa asilimia 90 ya mwewe barani ulaya.
Tangu wakati huo wanasayansi wamegundua upungufu wa ghafla wa mwewe waonavuka na kuingia nchini Ureno.
Uchunguzi wao unaonnyesha kuwa hali hiyo imetokana na uwepo wa mizoga badala ya mabadiliko ya hali ya hewa
DR TULIA TENA MBEYA LEO “YAWEZEKANA HATUWAFIKII KWA WAKATI”