Leo March 7, 2018 nimeipata stori kutoka nchini Afrika Kusini ambapo majambazi wamemvamia Mwanariadha nchini humo na kumtendea kitendo ambacho si chakiungwana baada ya kutaka kumkata miguu kabisa walipomshambulia wakati anafanya mazoezi alfajiri.
Polisi wanasema mwanaraidha huyo hakuwafahamu wanaume waliomshambulia lakini inavyoonekana ni kwamba shambulio hilo sio la wizi wa kawaida, na kwa hivyo maafisa wanachunguza uwezekano wa njama nyingine.
Mwanariadha Mhlengi Gwala mwenye umri wa miaka 26 anapatiwa matibabu katika hospitali moja huko Kwa Zulu-Natal baada ya kushambuliwa na wanaume watatu katika mji wa pwani Durban.
Haijulikani dhamira ya shambulio hilo lakini polisi wanasema mwanariadha Gwala aliwapa washambuliaji simu na pesa alizokuwa nazo, ambao badala yake walimsukuma chini na kumburura katika kichaka kilichokuwa karibu na kujaribu kumkata miguu yake kwa kutumia msumeno usiokuwa na makali.