Staa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Calvin Cordozar Broadus ambaye wengi wanamfahamu kwa jina maarufu kama Snoop Dogg alitangaza kuachana na muziki wa Hip Hop (kidunia) na kumrudia Mungu kwa kuanza kufanya nyimbo za dini.
March 16 Snoop Dogg ameachia rasmi album ya nyimbo za injili inayokwenda kwa jina la ‘Bible of Love’ mkongwe huyo katika muziki wa Hip Hop March 16 ameachia album yake hiyo ya gospel, baada ya kufanya muziki wa kidunia na kutoa jumla ya album 15 za Hip Hop, Snoop anafanya maamuzi hayo akiwa na umri wa miaka 46 sasa.
Album mpya ya Snoop Dogg alioitoa March 16 ‘Bible of Love’ amewashirikisha wasanii mbalimbali kama Pattie Labelle, Rance Allen, The Clark Sisters, Faith Evans, Kim Burrell, B. Slade Charlie Wilson, Marvin Sapp, Tye Tribbett, James Wright Chanel, Isaac Carre, Fred Hammond, Chris Bolton, Uncle Chuce, John P. Kee, Mali Music, Mary Mary, Lonnie Beareal na Jazze Pha.
Hii ni moja kati ya nyimbo zake zilizomo kwenye album ya “Bible of Love”
EXCLUSIVE: Sababu za Millen Magese kuchelewa kuonesha picha za mtoto wake ‘Kairo’