Baada ya wiki kadhaa kupita toka club za Yanga na Singida kucheza mchezo wa robo fainali ya Kombe la ASFC katika uwanja wa Namfua Stadium na Yanga kutolewa kwa mikwaju ya penati ila leo wamecheza kwa mara ya tano na kabla ya mchezo wa leo Yanga na Singida walikuwa wamecheza mara nne, sare mbili na kila mmoja kupoteza mmoja dhidi ya mwenzake.
Leo April 11 2018 Yanga na Singida Uwanja wa Taifa Dar es Salaam walikutana tena katika mchezo wa marudiano wa round ya pili ya Ligi, baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa mwaka jana na kumalizika kwa kutokuwa na mbabe kwa timu zote kutoka sare tasa.
Mchezo wa leo uwanja wa Taifa ulianza kwa presha za nje ya uwanja kwa makomando wa timu zote mbili kugombana kwa kuhofia kufanyiana hujuma, kitu ambacho kimewafanya hata Singida kutotumia chumba cha ugenini cha kubadilishia nguo kilichozoleka kutumika uwanja wa Taifa.
Ushindani wala mzozo wao wa nje ya uwanja haukuweza kuisadia timu yoyote kupata matokeo na mwisho wa siku, game ikamalizika kwa kufungana goli 1-1, goli la Singida likifungwa dakika ya 2 ya mchezo na Papy Kambale lakini Yanga walisawazisha dakika za nyongeza kipindi cha kwanza kupitia kwa Abdallah Shaibu ‘Ninja’.
VIDEO: Canavaro baada ya game amezungumzia ishu ya kustaafu