Wanasema kwenye maisha ya sasa chochote kinachokuja mbele yako usikichukulie poa na ni bora ujaribu kukipata ukikose kuliko kuacha kujaribu kabisa alafu kumbe ungeweza kushinda.
Kutana na Juma Athumani, kijana wa Kitanzania ambae ameajiriwa kwenye kijiwe cha kufetua tofali, alijikuta tu anazo shilingi elfu 3 kwenye simu yake na akaamua kujinyima na kutoa shilingi elfu moja kati ya hizo 3 na kucheza Bahati Nasibu mpya ya Taifa iitwayo TATU MZUKA.
Kweli maisha sio kukariri…. niliposikia jamaa Mfetua Tofali kashinda milioni 55 imebidi nimsikilize kwa makini ilikuaje?? >>> “Nashukuru uongozi wa TATU MZUKA kwa kutuwezesha sisi vijana ambao hatujui wapi pa kutokea na kupatia pesa, nimepata pesa kwa njia ambayo sikuitegemea kabisa”
“Siku ya kwanza nilipocheza TATU MZUKA nilitoa shilingi elfu mbili sikushinda, nikacheza tena kwa kuweka elfu 2 nyingine ikaliwa, nikafikiria kama kukata tamaa lakini haikua hivyo nikatoa tena pesa nyingine, siku ambayo nimekuja kushinda ni siku nimetoa shilingi elfu 1 kati ya shilingi elfu 3 nilizokua nazo kwenye simu”
“Usiku nikiwa nimetulia nikashangaa nimepigiwa simu na mtu akijitambulisha anatokea TATU MZUKA, akanipa hongera na kunipa simu niongee na watu wengine kutoka TATU MZUKA wakawa wananipa hongera… namshkuru sana Mungu“
“Kabla ya kufanya kazi yangu ya kufetua tofali nilikua Mwanafunzi wa ufundi wa kuchomelea lakini ilibidi nifanye kazi ya tofali sababu sikuwa na uwezo wa kununua vifaa vya kuchomelea lakini sasa hivi ndoto yangu imetimia” – Juma
Sebastian Maganga ambae ni Mratibu wa Mawasiliano wa TATU MZUKA amesema Jumapili hii mtu mmoja mwenye bahati ataondoka na SHILINGI MILIONI 100 ambapo pamoja na kwamba inasubiriwa hiyo Jumapili, bado kuna fursa za kila siku ndani ya kila saa ndani ya saa 24 kushinda shilingi milioni 6, tazama zaidi hii video hapa chini