Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa pamoja na yeye kukulia katika umasikini na mazingira ya shinda, watoto wake kwa sasa wanaishi kifahari hususani mtoto wake wa kwanza Cristiano Ronaldo Junior lakini lazima atamfundisha afahamu kuwa duniani kuna maisha ya shida pia.
Ronaldo katika mapumziko ya kipindi hiki cha majira ya joto alisafiri na mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior na kumuonesha nyumba aliyokuwa anaishi Lisbon Ureno “Wakati wa hii likizo nilienda na Junior katika nyumba niliyokuwa naishi Lisbon, alishangaa na kuniuliza baba ni kweli ulikuwa unaishi hapa? hakuamini, sio kipaji ndio kinakufuata wewe unatakiwa wewe ndio ukifuate hivyo ndio namna nilivyomfanya aelewe”>>> Ronaldo
Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji soka waliowahi kupitia maisha magumu kabla ya kufanikiwa kwao na kuna wakati ilimlazimu kushea chumba kimoja na dada zake kwa ajili ya kuwa na hali mbaya kiuchumi, umri ambao hakupaswa kushea chumba na dada zake, Ronaldo alifukuzwa shule kwa kosa la kumpiga na kiti mwalimu ndipo mama yake akamuambia sasa tia nguvu katika soka.
VIDEO: Kwa tathmini hii ya Edo Kumwembe, Mashabiki wa Chelsea haina budi kuwa wavumilivu