Ni kawaida kupewa tahadhari kwamba bongo ukiacha simu yako ovyo kama kwenye kituo cha daladala, baa, kwenye daladala, hotelini, kwenye gari binafsi na sehemu nyingine yoyote inaweza kuibwa ndani ya dakika sifuri.
Unaweza kuhisi labda hii tabia iko bongo tu au kwenye nchi masikini peke yake kitu ambacho sio sahihi aisee manake huko Marekani takwimu za utafiti wa mwaka 2013 peke yake zinaonyesha ni simu zaidi ya milioni 3 zilizoibwa kwenye taifa hili lenye watu zaidi ya milioni mia tatu.
Hiyo milioni tatu ni karibu ya mara mbili ya mwaka 2012 ambapo zillibwa milioni 1.6 ambapo unaambiwa kutumika kwa namba za siri katika smartphones pia kumekuwa na ongezeko la asilimia 50 mwaka 2013 lakini bado watu wengi hawajataka kutumia neno la siri lenye kuzidi tarakimu nne au applications ambazo zinaweza kugundua simu zao zipo wapi baada ya kuibwa.
Smart phones zilizoibwa kati ya hizi zinafikia milioni 1.4 na hazikupatikana ambapo mwaka 2012 ziliibiwa milioni 1.2 kwa hiyo wizi umeongezeka.
Hii video hapa chini sio ya Marekani, nimeitoa kwenye instagram ya @millardayo imefanywa na mchekeshaji Mganda, nyingine za muendelezo wake baada ya kurudi kumfata mwizi zipo hapohapo instagram @millardayo