Leo ni July 10, 2017 ambapo kama ulipitwa na story zote kubwa kwenye magazeti ya Tanzania asubuhi ya leo kupitia Televisheni, Radio, Magazeti au Mitandao mbalimbali ya kijamii nimekukusanyia na kukusogezea hapa kupitia millardayo.com.
Rais mstaafu Benjamin Mkapa amewataka Watanzania kubuni miradi itakayosaidia kuondokana na utegemezi wa mataifa yaliyoendelea. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi kimewafukuza wanafunzi 24 kwa makosa ya mimba, ulevi, utoro na wizi. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Mbunge wa Malindi, Z'bar Ally Saleh (CUF) amefungua kesi Mahakama Kuu DSM dhidi ya Rita kupinga usajili wa Bodi ya Wadhamini. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Imeelezwa kuwa upungufu wa vifaatiba na dawa ktk Hospitali ya Mkoa wa Rukwa hukwamisha juhudi za madaktari kutoa tiba kwa wagonjwa. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema ktk miezi mitatu iliyopita limekagua sampuli 180 za bidhaa mbalimbali kubaini ubora. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Dereva na Kondakta wa basi la Kampuni ya Bunda Express wanashikiliwa na Polisi kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Kampuni ya Acacia imepunguza wafanyakazi 200 ktk mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinganya. 100 kati yao kutoka Idara ya Ulinzi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Imeelezwa kuwa wanafunzi wanaobeba mimba shuleni ni wale wanaosoma shule za Serikali na wanaotoka katika familia masikini. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Serikali imesisitiza uamuzi wake wa kuendelea na mpango wa kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme ktk maporomoko ya Mto Rufiji. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Bohari ya Dawa (MSD) imetangaza kubadili vifungashio vya dawa kutoka makopo hadi blister Park kuzifanya dawa kuwa salama zaidi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Shirika la Umeme (Tanesco) limesisitiza azma ya kutumia nguzo za umeme za zege ili kuboresha huduma ya usambazaji wa umeme. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Rukwa imemhukumu Oscar Msangawake (53) kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kulima bangi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Vijana wametakiwa kuacha tabia ya kuiga utamaduni unaodhalilisha utu wao badala yake waige vitu vitakavyowaletea sifa na heshima. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Serikali imeombwa ichunguze Hospitali ya Igunga kubaini wauguzi waliozembea na kusababisha kifo cha mjamzito na mtoto wake. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Wenyeviti saba wa CUF, Unguja, wamesema njama ovu za kukihujumu chama hicho zinazofanywa na Prof. Lipumba hazitafanikiwa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Watumishi 6 Lindi, wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya taarifa za ubadhirifu wa fedha iliyotolewa na CAG 2015/16. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Mtandao wa Haki za Binadamu, utafungua kesi ya kikatiba kupinga Polisi kuzuia maandamano ya amani waliyotaka kufanya July 6. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa anaanza ziara ya wiki moja katika Mkoa wa Lindi kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Mkoani humo. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Rais mstaafu Mkapa leo atakabidhi nyumba 10 kwa ajili ya Hospital ya Wilaya ya Chato, Geita zilizojengwa na Mkapa Foundation. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Mtoto mchanga amenusurika kufa baada ya kutumbukizwa chooni na mama yake mzazi, baada ya kujifungua Mkoani Singida. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Rais mstaafu Benjamin Mkapa amewataka Watanzania kubadili fikra na mtazamo kwa kubuni miradi itakayosaidia jamii, Taifa kujitegemea. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Wanawake nchini wametakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kujiongezea kipato na kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Ma-RC na Ma-DC wametakiwa kutenga maeneo maalumu kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maeneo ya viwanda kwa wajasiriamali wadogo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Mtanzania aliyekataa mshahara wa Tsh. Milioni 425 Marekani amerejea nyumbani!!!