Nchini Kenya, takriban watu 41 waliookolewa katika sakata la mauaji la msitu wa Shakahola, mjini Kilifi pwani ya nchi hiyo, sasa watafunguliwa mashtaka ya mauaji.
41 hao pamoja na kiongozi wao muhubiri mwenye utata paul mackenzi watashtakiwa kwa mauaji ya baadhi ya watu wa família zao.
Waendesha mashtaka nchini humo wanasema waathiriwa hao waliogeuka kuwa ashukiwa walikuwa wazazi wa watoto waliofariki au kutoweka, na kwamba walikuwa na hatia kwa kile kilichotokea.
Kiongozi wa Mackezi, naye anatuhumiwa kwa kuwahimiza wafuasi wake kususia chakula hadi kufa iwapo walitaka kukutana na yesu kabla ya dunia kuisha.
Hadi kufikia sasa polisi wanaoendesha uchunguzi wa mauaji hayo wamafukua miili zaidi ya 400 kutoka kwenye msitu wa shakahola, huku watu wengine 600 wakiwa bado hawajapatikana.