Uchunguzi mpya uliofanywa nchini Marekani unaonyesha mmoja kati ya wafungwa 25 wa mauaji hakufanya kosa hilo hivyo zaidi ya asilimia 4 kati ya wafungwa wa kimarekani wamehukumiwa kifo lakini hawakutenda makosa hayo.
Wachunguzi kutoka Pennsylvania, Michigan na kwengineko wamekaa pamoja kuchunguza kitu kinachoitwa “Dark figure” yaani hesabu ya wafungwa waliohukumiwa kifo na wakati hawakufanya uhalifu unaowafanya wahukumiwe kifo.
Matokeo ya uchunguzi huo ambayo yalichapishwa na (National Academy of Science of the United States) yameonesha kuwa mauaji ya watu wasio na hatia yamekua kitu cha kawaida nchini humo.
Walionyongwa/kuuliwa bila ya hatia wamezidi kutoka asilimia 1.6 mpaka asilimia 4.1 ambapo wafungwa 340 walikuwa wawe wameshatolewa ndani ya miaka 30 iliyopita na 138 kati yao walinusurika na adhabu hiyo.
Wengi walinusurika na adhabu hiyo kati ya miaka ya 1993 mpaka 2004 ambapo watu 2,675 walitolewa katika orodha ya kuuliwa baada ya uangalizi wa makini kufanyika tena katika kesi zao ambapo hiyo ni asilimia 36 ya watu waliokutwa na adhabu hii kati ya miaka hiyo.
Hata hivyo hawakuachiwa huru pamoja na kwamba waliondolewa adhabu ya kunyongwa badala yake walipewa adhabu nyingine na wengi wao wakihukumiwa kifungo cha maisha.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? jiunge na mimi twitter instagram na facebook kwa jina la @millardayo ili niwe nakutumia kila zinaponifikia iwe usiku au mchana.