Toka March 8 2014 mpaka leo ikiwa ni May, ndege ya Malaysia iliyokua imebeba zaidi ya watu 200 haijulikani ilipo baada ya kupotea ikiwa inatokea Malaysia kwenda Beijing China.
Kwa siku zote hizo toka imepotea ndugu wa abiria wa ndege hiyo wamekua wakishinda kwenye hoteli ambazo pia zimekua zikitumiwa na shirika hilo la Malaysia kukusanyika na kutoa taarifa kuhusu kinachoendelea kwenye kuitafuta ndege hiyo.
May 1 2014 taarifa zimeanza kusambaa kwamba ndugu hao sasa wamepewa maagizo waondoke kutoka kwenye hoteli zote walizofikia Beijing na Kuala Lumpar na kurudi nyumbani kwao ambapo taarifa za chochote kitakachotokea watazipata wakiwa hukohuko majumbani.
Hii iliwafanya ndugu kadhaa kuangua tena vilio na kupiga mayowe baada ya kujua kwamba taarifa ya shirika hilo la ndege inamaanisha haitakuwepo tena ile mikusanyiko ya kila siku kwenye chumba cha mikutano kwa ndugu hao kupewa taarifa za kinachoendelea kwenye zoezi la utafutaji wa ndege hiyo.
Kwenye hoteli ya Lido Beijing ambako kampuni hiyo ya ndege imekua ikiwalipia ndugu hao wa abiria toka ndege ipotee, kulikua na watu wanaozidi 500 ambao wote ni ndugu wa abiria waliopotea.
Hata hivyo kampuni hii ya ndege itaanza kutoa malipo ya pesa kwa ndugu hao siku za karibuni ambapo japo haijasema itatoa kiasi gani, sheria inasema ndugu wanaweza kulipwa kuanzia dola za kimarekani laki moja na nusu mpaka laki moja na elfu 75.
Ripoti mpya iliyotoka inasema maafisa hawakua wamegundua kupotea kwa ndege hiyo mpaka dakika 17 baadae na walichelewa kwa dakika 240 kuanza kuitafuta ndege hiyo baada ya kupotea kwenye radar.
Ili kutumiwa kila taarifa inayonifikia, karibu ujiunge na mimi kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la @millardayo na nitafanya hivyo iwe usiku au mchana.