Najua hata bongo hii huwa inatokea pale mnapokua Wapangaji kwenye nyumba moja au majirani alafu chumba cha jirani kila siku unasikia nyimbo za msanii mmoja tu tena zinapigwa kwa sauti kila jamaa akiwemo ndani.
Mamlaka ya usalama ya Uingereza imemkataza raia mmoja wa nchi hiyo aitwae Gareth Davies kutosikiliza wimbo wa Celine Dion wa ‘My heart will go on’ baada ya malalamiko kutoka kwa majirani kwamba amekua akirudia kuucheza wimbo huo kwa sauti kubwa siku nzima.
Gareth amenyang’anywa vyombo vyake cha muziki baada ya malalamiko hayo ambavyo ni 3D TV,Laptop,Spika na hata Playstation 3 na alishapata barua ya kupunguza kelele kutoka Mahakamani mara 6 lakini bado aliendelea na kupiga mziki huo.
Davies mwenye umri wa miaka 47 ameruhusiwa kubaki na iPhone na MacBook yake lakini amekatazwa kabisa kupiga wimbo wa Celine Dion my heart will go on au mwengine wowote ule kwa sauti kubwa ambapo vitu vyake vilivyochukuliwa atarudishiwa baada ya muda wa siku 28.