Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amewataka Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri nchini kuboresha utendaji kazi kwa shule za msingi hasa katika ufundishaji wa lugha ya kiingereza kwani waliongia kidato cha kwanza 2022/2023, takwimu za Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) zinaonesha 71% Wanafunzi wahawana umahiri wa lugha ya Kiingereza
Dkt. Msonde ameeleza hayo kwenye Mkutano wa Tisa wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini, uliyofanyika Jijini Mwanza.
Kwa apande wake Kamishna wa Elimu nchini Dkt. Lyabwene Mutahabwa amewataka Walimu kuacha kutoa adhabu kali zinaweza kuhatarisha afya na maisha ya Mwanafunzi badala yake watumie mbinu zinazoweza kuwajenga kiufaulu na kimaadili kwani Mtoto ni rasilimali pekee ya thamani kwa Mwanadamu
Dkt. Mutahabwa ameongeza kwa kuwakumbusha Maafisa elimu kutoa nafasi ya kuwasikiliza waliochini yao na sio kutoa maelekezo kulingana na vyeo vyao bila ya kujali utu
Mkutano wa kuwakutanisha Maafisa elimu wa Mikoa na Halmashauri nchini hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwakumbusha utendaji kazi wao ili kuongeza ufanisi wa elimu nchini.