Tangu kuzinduliwa kwa mtandao wa Instagram mwaka 2010, jukwaa hilo limefanya mabadiliko makubwa lakini hakuna ambalo limezua utata zaidi ya mfumo wake wa hivi karibuni kuipa kipaumbele maudhui ya video zaidi ya picha.
Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Instagram Adam Mosseri, muda unavyozidi kusonga mbele, jukwaa la Instagram litatawaliwa na video zaidi ya picha “Ukiangalia maudhui ambayo Watu wanapenda kutazama na wanayoshiriki kwenye mtandao wa Instagram inaonesha mwendendo unaotawaliwa na video zaidi ya picha na mabadiliko haya yangetokea bila hata ya sisi kubadilisha chochote, itabidi tuegemee kwenye mabadiliko hayo huku tukiendelea kuunga mkono maudhui ya picha”
Mjadala huu ulizuka baada ya Wanawake wawili wenye Wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram duniani Kylie jenner pamoja na Dada yake Kim Kardashian kupost picha kwenye kurasa zao, iliyopata zaidi ya likes million mbili, iliyoandikwa “Make Instagram, Instagram again, Stop trying to be TikTok, I just want to see cute photos of my friends, Sincerely, everyone” wakimaanisha “Fanyeni Instagram, iwe Instagram tena, acheni kujaribu kuwa TikTok, ninachotaka ni kuona picha nzuri za marafiki zangu tu; Kwa dhati, kila Mtu”
Post hi ilikuwa ujumbe wakumfikia CEO wa Instagram, kuonesha kipangamizi dhidi ya mfumo mpya wa mtandao huo kufanana na ule wa mtandao wa Tiktok, ambao umetaliwa na video zaidi ya picha kama ilivyokuwa awali katika mtandao huo wa kijamii, Kylie Jenner kwa siku moja, alipunguza hisa za mtandao wa Snapchat kwa kiasi cha $1.3bilioni kwa sababu alisema hakufungua application hiyo tena baada ya wao kubadilisha mfumo wao, hii inaonyesha jinsi gani anaushawishi mkubwa mitandaoni.