Shirika la Wanyama Duniani (WWF) limezindua programu ya kurudisha uoto wa asili na misitu katika nchi za 10 za Afrika huku ikilenga kupanda miti milioni 2.6 nchini hadi kufikia mwaka 2027.Programu hiyo itafanyika kaa miaka mitano kuanzia sasa hadi mwaka 2027.
Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Dk Amani Ngusaru ambaye ni Mkurugenzi wa WWF Tanzania amesema upandaji wa miti unaofanyika nchini unaunga mkono jitihada za Serikali.
“Serikali imedhamiria kupanda miti milioni 5.2 hadi mwaka 2030, sisi kama WWF yutakwenda kupanda nusu ya malengo yao hadi kufikia mwaka 2017, tunataka kurejesha uoto wa asili ambao unapotea,” amesema
Miti hiyo imekuwa ikipotea kutokana na kukatwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo matumizi kama nishati ya kupikia, kilimo na uwindaji wa kutumia moto.
Kwa mujibu wa takwimu, hekta milioni 10 za misitu hukatwa kila mwaka duniani kote, kwa upande wa Afrika hekta milioni nne hupotea kila mwaka huku Tanzania ikipoteza hekta 469,000 kila mwaka.
Dk Ezekiel Mwakalukwa ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii amesema programu hiyo ni muhimu katika kurejesha uoto wa asili uliopotea ambayo pia itasaidia kupunguza athari za mbadiliko ya tabia nchi.
“Tunapoharibu misitu tunapoteza vyanzo vya maji kusababisha hewa ya ukaa angani inayoleta joto au kusababisha mvua zisizokuwa na mpangilio maalumu, Serikali pia imejipanga ili kuhakikisha lengo la upandaji miti iliyojiwekea linatimia”–