Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la moto ulioteketeza Bar ya Amsterdam Mbezi Beach usiku wa September 13, 2022.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni SACF, Christina Sunga amesema.. “Zimamoto walipofika mooto ulikuwa mkubwa kwasababu ni eneo ni la biashara na unaona lipo katikatika ya Makazi ya Watu lakini aina ya ujenzi uliokuwa umejengwa Bar hii ni aina ya makuti, wamejenga kwa kutumia miti na makuti na ilikuwa Bar yenye floor kwa maana chini na juu lakini eneo hili hasa limeathirika kulipokuwa na makuti”- Christina Sunga
“Kuna fremu takribani 7 za maduka yaliyoweza kuokolewa na kuna majiko ya chakula vyumba takribani vitatu ambavyo havikupata madhara, hivyo eneo kubwa lililopata madhara ni eneo la Bar” – Christina Sunga