Kwenye headlines za Kenya wiki hii na hii imo manake kauli za mamlaka husika zimepishana huku upande huu ukisema ni marufuku magari yote ya abiria na binafsi kuendelea kuwa na vioo vyeusi (tinted) nchini Kenya huku upande mwingine ukisema marufuku hiyo ni kwa magari ya abiria tu ikiwa ni jitihada za kuhakikisha magaidi hawajifichi.
Hii ishu ilifanya mpaka mwananchi mmoja aitwae Alachi Okala kwenda kufungua kesi Mahakamani kwa kitendo hicho ambacho aliona kimevuka mipaka kwenye uhuru wa kila mwananchi.
Baada ya hilo, hatimae Mahakama kuu kenya imetoa amri ya kuzuia magari binafsi kuondolewa vioo hivyo na kwamba agizo la kuondoa tinted liendelee kwa magari ya abiria peke yake.
Stori kama hizi ni halali yako zisikupite…. ili niwe nakutumia kila kinachonifikia ungana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, kama upo Facebook na Instagram pia unaweza kubonyeza FB na INSTA ili kupata kila stori inayonifikia zikiwemo videoz, vituko, pichaz, music na mengine yote.