Puto la kijasusi la kutokea China lililoonekana nchini Marekani mapema mwaka huu liliweza kunasa picha na kukusanya taarifa za kijasusi kutoka kwenye tovuti za kijeshi za Marekani, chanzo kinachofahamu suala hilo kiliiambia CNN.
Puto hilo liliweza kuchukua taarifa na kuzifikisha nchini China na serikali ya Marekani bado haina uhakika kama serikali ya China inaweza kuzitumia taarifa zilizokusanywa na puto hilo na jambo hilo linazua maswali mengi kuhusu taarifa za kijasusi ambazo puto hilo liliweza kukusanya ambazo Marekani bado haizijui. Mpaka sasa jumuiya ya ujasusi nchini Marekani haijahakikisha tetesi za kuwa puto hilo liliweza kukusanya taarifa nyeti zisizojulikana kwa sababu teknolojia inayoitumia sio ya kisasa zaidi kuliko yale ambayo satelaiti za China zinaweza kukusanya zinapozunguka maeneo sawa.
Kama ilivyoripotiwa na CNN, jumuiya ya kijasusi ya Marekani mwaka jana ilibuni mbinu ya kufuatilia kile inachosema ni vikundi vya Maputo haya ya China zinazofanya kazi kote ulimwenguni, zinazodhibitiwa na jeshi la China.
Shirika la kijasusi la nchini Marekani FBI bado inachunguza puto hilo lakini hadi sasa maafisa wameweza kukusanya maelezo ya ziada kuhusu jinsi kifaa kilifanya kazi ikiwa ni pamoja na kanuni za algoriti zinazotumiwa kwa programu ya puto na jinsi inavyoendeshwa na kuundwa. CNN imefikia Baraza la Usalama la Kitaifa katika Ikulu ya Marekani na Pentagon kwa maoni. NBC ilikuwa ya kwanza kuripoti juu ya ujasusi huo.
Puto hilo lilirushwa kwa mara ya kwanza kwenye anga ya Marekani jijini Alaska mwishoni mwa mweziJanuari kabla ya kupitia Canada na kushuka hadi jimbo la Montana, ambako ilitanda kwa siku chache na kusababisha Marekani kuamini kuwa ilikuwa inajaribu kuchunguza maeneo nyeti ya kijeshi, kama Kituo cha Jeshi la Anga la Malmstrom huko Montana. Hatimaye ilitunguliwa na Marekani kwenye Pwani ya Mashariki mnamo Februari 4 na tukio hilo lilizidisha mvutano kati ya Marekani na China ikiwa ni pamoja na kuahirishwa kwa ziara ya kidiplomasia ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken nchini China.