Barua pepe zilizofichuliwa na kampuni ya gesi ya Ukraine zinaonyesha kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden na mwanawe walishiriki katika utakatishaji fedha wa kampuni hiyo.
Barua pepe zilizopatikana zinaonyesha kuwa kampuni ya gesi ya Ukraine Burisma ilimwajiri mtoto wa rais wa sasa wa Marekani, Hunter Biden, mwaka 2014 na kuanzisha naye akaunti ya pamoja huko Malta, ambayo baadaye ilifungwa kufuatia uchunguzi wa uhalifu wa kifedha.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Hunter Biden, mtoto wa Rais wa Marekani, Joe Biden na kampuni ya gesi ya Ukraine wameshiriki kuunda akaunti katika benki ya kigeni ambayo ilifungwa baada ya uchunguzi wa utakatishaji wa fedha chafu.
Siku ya Jumanne mtoto wa rais wa Marekani , Hunter Biden, alifikia makubaliano na Idara ya Sheria ya kukiri mashtaka matatu ya kukwepa kulipa kodi na kumiliki silaha kinyume cha sheria, ambayo yanaelezwa kama yanayopunguza uwezekano wake kufungwa gerezani.
Kulingana na kesi iliyowasilishwa mahakamani siku ya Jumanne, Hunter Biden, mwenye umri wa miaka 53, ambaye kwa muda mrefu ametatizwa na uraibu wa mihadarati na uchunguzi wa shughuli zake za biashara nje ya nchi, atakubali mashtaka mawili ya makosa ya kukosa kulipa kwa wakati, kati ya mwaka 2017 na 2018, na kukubali kuwekwa katika hali ya uangalizi, maarufu probation.
Nyaraka za mahakama zilionyesha kwamba Idara ya Sheria ilikubali kutomfungulia mashataka kuhusiana na ununuzi wake wa bunduki mnamo mwaka wa 2018 alipokuwa akitumia dawa za kulevya, ingawa alidai kwenye hati ya ununuzi kuwa hakuwa anatumia dawa hizo.