Nchini DRC, wanasiasa, hasa kutoka upinzani, wanasubiri kuanza kwa mikutano iliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) chini ya miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu.
Tangazo hili la CENIi linakuja baada ya miezi kadhaa ya maandamano kutoka kwa upinzani na sehemu ya mashirika ya kiraia ambao wanalaani kutokuwepo kwa uwazi katika uendeshaji wa mchakato wa uchaguzi.
Mikutano inapaswa kuwezesha, kulingana na Mwenyekiti wa CENI, Denis Kadima, kutafuta “suluhu za kweli kwa mchakato unaojumuisha zaidi”.
Upinzani unatarajia mengi kutoka kwa mijadala hii. Kwa upande wa upinzani, Martin Fayulu anatumai kuwa CENI itakubali uundwaji upya wa orodha za wapiga kura na ukaguzi wao. Mkutano huu, anabaini, bado unapaswa kutumika kuweka mfumo wa “kupitia upya pamoja sheria”.