Rais wa Iran Ebrahim Raisi anaendelea na ziara yake ya kwanza barani Afrika, ambayo Tehran inalenga kuitumia kupanua uhusiano wa kisiasa na kiuchumi katika bara zima.
Raisi alipangiwa kuondoka Tehran siku ya Jumanne kwa safari ambayo itampeleka Uganda na Zimbabwe katika safari ya kwanza ya rais wa Iran barani Afrika katika kipindi cha miaka 11.
Raisi alizuru Kenya mara ya kwanza asubuhi na kisha katika nchi jirani ya Uganda mchana ambapo alikutana na mwenzake Yoweri Museveni na kupata fursa ya kuunga mkono masuala kadhaa, kuanzia sheria ya “kupinga ushoga ya mwaka 2023” iliyotangazwa Mei 29 na Kampala.
“Nchi za Magharibi zinajaribu leo kuendeleza wazo la ushoga, na kwa kulikuza, wanajaribu kukomesha aina ya binadamu,” amesema rais wa Iran Ebrahim Raïsi: Rais wa Irani alizungumza kutoka Kampala, mwezi mmoja na nusu baada kutangazwa kwa sheria ya “kupinga ushoga” ambayo ilikuwa na uhusiano mbaya kati ya Uganda na washirika wake wa Magharibi.
Yaliyomo katika sheria hiyo yanachukuliwa kuwa moja ya kandamizi zaidi ulimwenguni: inatoa adhabu ambayo inaweza kwenda hadi adhabu ya kifo na inakataza “kuendeleza” kwa ushoga.
Mnamo Mei 29, saa chache baada ya sheria hii mpya, nchi kadhaa, pamoja na Marekani, ziliahidi mara moja vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Uganda.
Kutokana na mfululizo huu wa misimamo ya Magharibi, Kampala ilionysha msimamo wake: “Nchi za Magharibi hazitakuja kutawala nchi yetu”, alitangaza spika wa bunge la Uganda. Siku ya Jumatano, rais wa Iran kwa alionyesha uungaji wake mkono kwa mwenyeji wake, Rais Museveni akithibitisha kwamba “nchi za Magharibi zinafanya kinyume na urithi wa tamaduni na mataifa”.
Rais wa Iran, alizungumza siku ya jana asubuhi mjini Nairobi na mwenzake wa Kenya William Ruto, kisha aliwasili alasiri huko Entebbe nchini Uganda na anatarajiwa kusafiri hadi Harare nchini Zimbabwe siku ya Alhamisi kukutana na Rais Emmerson Mnangagwa.