Amekua ni miongoni mwa vijana wachache wa Tanzania wanaojituma lakini pia waliotoka mbali tena kwenye biashara iliyokua ikimpa kipato kidogo lakini leo anatajwa na jarila la Marekani la Forbes kuwa miongoni mwa vijana matajiri Africa.
Patrick Ngowi alianza kwa kuuza vocha enzi hizo lakini kwa sababu alijua nini anataka, alijipanga mpaka akafika hapa alipo ambapo kazi yake kubwa ni usambazaji wa umeme wa jua au solar ambazo kampuni yake imekua ikizifunga sehemu mbalimbali.
Kwa yeyote anaeifahamu historia ya Ngowi ataamini kwamba kazi kwa bidii, kutokukata tamaa, mipango, nidhamu na kuweka nguvu kwenye ndoto inaweza kubadilisha maisha ya yeyote yule.
Kupata nafasi ya kuhojiwa na kituo cha CNN sio kitu kidogo kabisa, ni miongoni mwa vituo vichache vikubwa vya habari duniani.
Moja kati ya vitu alivyoviongea nikaona ni vikubwa na vinabadilisha maisha ya Watanzania wengi, Patrick alisema umeme wake wa jua unabadilisha maisha ya watu wengi mfano kina mama au Wafanyabiashara wenye maduka kijijini na sehemu nyingine ambao walikua wanafunga maduka yao saa kumi na mbili jioni kwa sababu hakuna umeme lakini baada ya kufungiwa solar wanafanya kazi mpaka saa nne usiku na kuendelea.
Hiyo pekee kwa harakaharaka inakuza uchumi wa mwenye duka lakini pia wa serikali.
Ngowi anakua Mtanzania wa pili kuhojiwa na CNN ndani ya wiki mbili ambapo kabla yake alihojiwa Mwanariadha wa zamani Filbert Bayi.
Stori kama hizi ni halali yako mtu wangu, millardayo.com ina kazi ya kuhakikisha hupitwi hivyo ili kuwa karibu zaidi na kila kinachonifikia, jiunge na mimi kwa kubonyeza twitter facebook na instagram ili niwe nakutumia kila kitu.