Rais wa Niger Mohamed Bazoum ameapa kulinda vikali mafanikio ya kidemokrasia “yaliyopatikana kwa bidii” baada ya kushikiliwa na kikosi maalum cha walinzi wa rais ambacho kilitangaza kwamba kimechukua madaraka.
Shirika la habari la@DW liliripoti kuwa Rais Bazoum alishikiliwa mjini Niamey siku ya Jumatano na wanajeshi wa kikosi maalumu cha ulinzi wa rais ambao baadae walitangaza kwamba wamechukua madaraka.
Katikati mwa miito ya kulaani mapinduzi hayo kutoka Jumuiya za kikanda na kimataifa, Rais Bazoum ameonekana kushikilia msimamo wake kwamba yeye bado ni rais wa taifa hilo. Kupitia mtandao wa Twitter ambao hivi sasa unajulikana kama X, aliandika kwamba “maendeleo yaliyopatikana kwa bidii yatalindwa”.
Naye waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo Hassoumi Massoudou katika mahojiano na kituo cha Runinga cha France 24 alisema kuwa “madaraka ya kisheria na halali” nchini Niger ni yale yanayotekelezwa na rais aliyechaguliwa. Ameeleza kuwa Rais Bazoum “yuko na afya njema” na kwamba kulikuwa na “jaribio la mapinduzi” lakini si “jeshi lote limehusika”.
Usiku wa kuamkia leo, viongozi wa mapinduzi walijitokeza kupitia Televisheni na kutangaza kwamba wanasimamisha “taasisi zote” na kuanzisha hatua nyingine ikiwemo kufunga mipaka ya nchi na marufuku ya kutotoka nje usikuhadi pale watakapotoa “taarifa nyingine”. Kanali Meja Amadou Abdramane, ambaye ni msemaji wa Kamati ya kitaifa ya wokovu wa watu CNSP akiongozana na wanajeshi wengine 9 waliovalia sare za kijeshi alisema kuwa.