Chuo Kikuu Ardhi kupitia mradi wa HEET kinamipango ya kuanza rasmi ndani ya miezi 18 ya ujenzi wa majengo ambayo ni madarasa, yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 4,604, Maabara Mtambuka , yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi , Studios, zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 780, karakana za ufundi majengo zenye uwezo wa kuchukua 492 kiwa ni moja ya mageuzi katika élimu ya juu nchini.
Hii leo chuo hicho pia kimesaini mktaba na kampuni ya ujenzi ya China Jiangxi International Economic and Technical Cooperation wa kuanza rasmi kwa ujenzi wa majengo hayo.
Lengo kuu la ujenzi huu ni pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 6,074 kwa sasa hadi kufikia 12,620 yani udahili unaoendana na maoteo ya Mpango wa Chuo (Corporate Plan) wa miaka Kumi , kuboresha walimu wanaokwenda kusoma na kurudi kufundisha wanafunzi, na ununuzi wa vifaa pamoja na uboreshwaji wa mazingira bora ya kusomea kwa wanafunzi.
Majengo hayo yote kwa jumla yatakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 6546 na walimu 93 kwa mkupuo.