Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anatazamiwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wa Bayern Munich kuhusu mustakabali wa Harry Kane leo, talkSPORT inafahamu.
Bayern walikuwa na ofa ya pauni milioni 70 kwa nahodha huyo wa Uingereza iliyokataliwa mapema mwezi huu lakini wanapanga dau lililoboreshwa.
Washauri wa Kane wamedai kuwa yuko tayari kujiunga na mabingwa hao wa Bundesliga.
Mshambulizi huyo, ambaye leo anatimiza miaka 30, ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake Tottenham na talkSPORT inafahamu kuwa havutiwi na mkataba mpya.
Levy anamthamini Kane kwa pauni milioni 100 na inafikiriwa kuwa Bayern wako tayari kulipa hadi pauni milioni 86.
Miamba hao wa Ujerumani wanaweza kusubiri kufikia makubaliano ya awali ya mkataba na Kane mwezi Januari kabla ya uhamisho wa bure – ingawa wanaweza kukabiliwa na ushindani mkubwa.
Paris Saint-Germain pia wana nia ya kumsajili Kane, wakati Manchester United wanaweza kujiunga tena ikiwa atapatikana bila malipo.
Mshambuliaji huyo wa Tottenham tangu hapo amempita Jimmy Greaves kama mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo akiwa na mabao 280 katika michuano yote.