Mwimbaji kutokea nchini Nigeria Wizkid bado anaomboleza kifo cha mamake, Bi Jane Dolapo Balogun ambaye alifariki mnamo Ijumaa, Agosti 18, karibu 1:30 asubuhi.
Meneja wa Wizkid, Sunday Are, alithibitisha habari hizo kwa waandishi wa habari wa Nigeria alisema, “Ndiyo, alikufa asubuhi ya leo, yapata saa 1:30 asubuhi.”
Mastaa wengi wametuma salamu zao za rambirambi kwa Wizkid, akiwemo Davido, Olamide, na Burna Boy.
Davido aliandika kwenye Twitter, “Praying for you my brother @wizkidayo,Sadness flies away on the wings of time.”
Olamide alitweet, “Prayers up for Wiz.”
Burna Boy, ambaye alikuwa akitumbuiza katika tamasha la Afro Nation nchini Marekani, aliwaomba watazamaji kutulia muda kidogo kwaajili ya kumkumbuka mamake Wizkid. Alisema, “Hebu tuchukue muda kuonyesha upendo wetu na msaada kwa Wizkid. Mama yake amefariki leo. Tumuombee.”