Licha ya kuripotiwa kifo cha bosi wa mamluki wa Urusi Yevgeny Prigozhin, Moscow ina nia ya kuendelea na shughuli za kundi lake la kijeshi la Wagner barani Afrika, wataalam waliambia AFP siku ya Alhamisi.
Urusi imekuwa ikitoa shughuli barani Afrika kwa Wagner tangu 2014.
Kwa upande wa usalama, wapiganaji wa Wagner wametumwa pamoja na majeshi ya kitaifa ya Libya, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mali.
Siku ya leo msemaji wa Putin Dmitry Peskov aliambia BBC kwamba madai ya Kremlin kutoa amri ya kumuua Yevgeny Prigozhin ni “uongo mtupu”.
Kauli imetolewa wakati wa simu ya mkutano kati ya waandishi wa habari na msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov leo.
Wakati wa simu hiyo, Peskov alimwambia mwandishi wa BBC Will Vernon “kulikuwa na uvumi mwingi” kuhusu ajali ya ndege na “kifo cha kutisha” cha abiria waliokuwemo.
Aliendelea, ‘Huko Magharibi bila shaka uvumi huu unatoka kwa pembe fulani. Yote ni uwongo kabisa. Bila shaka tunapozungumzia suala hili tunapaswa kuongozwa na ukweli tu.