Mkuu wa serikali ya Libya amemsimamisha kazi Najla al-Mangoush na amesimamishwa kazi kwa muda” na kutegemea “uchunguzi wa kiutawala” na tume inayoongozwa na Waziri wa Sheria, serikali ya Abdelhamid Dbeibah, inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, ilitangaza siku ya Jumapili jioni, kulingana na uamuzi rasmi uliochapishwa kwenye Facebook.
Siku ya Jumapili jioni, Baraza la Rais wa Libya (PC), chombo kilichopewa mamlaka fulani ya utendaji na kutokana na mchakato wa kisiasa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kiliomba “ufafanuzi” kutoka kwa serikali, kulingana na kituo cha televisheni cha Libya al-Ahrar, ikinukuu barua iliyothibitishwa na msemaji wa CP Najwa Wheba.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen alitangaza Jumapili Agosti 27 kwamba alikutana na mwenzake wa Libya Najla al-Mangoush wakati wa mkutano ‘wa kipekee’ huko Roma wiki iliyopita. Tripoli ilitaja mazungmzo kuwa “hayakuwa rasmi” na kwa bahati mbaya, waziri wa mambo ya nje amefutwa kazi.
“Nilizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya kuhusu uwezo mkubwa ambao uhusiano kati ya nchi hizo mbili unawakilisha,” Eli Cohen alisema, kulingana na taarifa kutoka ofisi yake. Waziri wa Israel alisema alijadiliana na Najla al-Mangoush “umuhimu wa kuhifadhi urithi wa Uyahudi wa Libya kupitia ukarabati wa masinagogi na makaburi ya Wayahudi katika nchi hii”.
Hii ni “hatua ya kwanza katika uhusiano kati ya Israel na Libya”, alisema waziri huyo, akizingatia kwamba “ukubwa wa Libya na nafasi yake ya kimkakati inatoa fursa kubwa kwa taifa la Israeli”. Mkutano huo ulifanyika chini ya uangalizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Antonio Tajani, kwa mujibu wa taarifa hiyo.