Mtu wa tatu amekamatwa na kushtakiwa kuhusiana na kifo cha mvulana wa umri wa miaka 1 ambaye alipatikana na dawa yenye nguvu ya fentanyl katika kituo cha kulelea watoto cha Bronx, ambapo kiasi kikubwa cha dawa hizo zilihifadhiwa chini ya sakafu ya chumba ambacho watoto walicheza na kulala, kulingana na waendesha mashtaka wa shirikisho.
Mamlaka ilimtambua mwanamume huyo kuwa Renny Antonio Parra Paredes, 38, na kumshtaki Jumatatu katika Mahakama ya Wilaya ya Manhattan kwa kosa moja la kula njama ya kusambaza mihadarati na kusababisha kifo.
Mnamo Jumatatu maafisa walisema walipata mihuri wakati wa upekuzi katika nyumba ya mshukiwa ambayo ilitumiwa kuweka alama za vifurushi vya dawa za kulevya.
Bw Paredes anashtakiwa kwa kula njama ya kusambaza mihadarati na kusababisha kifo.
Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DEA) inasema kuwa Bw Paredes alitekeleza jukumu muhimu katika oparesheni inayodaiwa kuwa ya ulanguzi wa dawa za kulevya uliofanyika katika kituo cha kulelea watoto cha Divino Niño.