Katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa kike duniani, mkoani Geita halmashauri ya mji Geita wamekuwa mstari wa mbele katika kuadhimisha siku hiyo ambapo mtoto wa kike ametakiwa kujitambua pamoja na kuachana na vishawishi ambavyo vimekuwa vikipelekea kurubuniwa kwa kuhongwa chipsi na kuharibu ndoto zao.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari nyanza iliyopo wilayani Geita afisa elimu shule halmashauri ya mji Geita ,Magreth Macha amesema chanzo cha kukatishwa ndoto za mtoto wa kike kimekuwa kikitokana na Mtoto mwenyewe kukubali vishawishi ikiwemo chips pamoja na Soda.
“Tujifunze kukataa vishawishi vishawishi vya Chipsi ,soda ,nyama choma vizawadi vidogo vidogo mpaka na vingine Tuache sawa Jamani ili tuvumilie kwenye shida na raha Baadaye tuweze kutimiza Malengo yetu , ” Afisa Elimu Mji Geita.
Bi.Macha ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa kata wakiwemo Maofisa Watendaji pamoja na wenyeviti wa Mitaa na Vitongoji kuhakikisha wanawakamata wale wote ambao wamekuwa wakitelekeza Familia kwa kisingizio cha Ugumu wa Maisha hasa kwa Maeneo ya Geita.
Kwa upande wake Msimamizi wa Masuala ya Jinsia kutoka Mradi wa KAGS kwa kushirikiana na Shirika la Plan International Bi.Heldgeda Mashauri amesema uwepo wa miradi katika kutetea Mtoto wa kike imesaidia katika jamii kuondokana na Unyanyasaji pamoja na mtoto wa kike kuonekana hana uwezo wa kuwa kiongozi.
“Wasichana wameweza kuwa Viongozi lakini wasichana wameweza kuongoza hii sherehe nzima kwa ujumla sisi kama Plan International kupitia mradi wa KAGS tunaendelea kuielimisha Jamii juu ya umuhimu wa elimu hasa kwa Msichana , ” Bi. Heldgeda.
Anastasia Alicen ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari kisesa Geita amesema uwepo wa miradi umeweza kuwasaidia watoto wa kike katika kukamilisha ndoto zao ikiwemo kuletewa vifaa vy akujifunzia pamoja na elimu ambayo wamekuwa wakipewa wakiwa Mashuleni.