Pale ambapo mastaa zaidi ya 100 wa Tanzania kwenye muziki na filamu pamoja na sehemu nyingine wamesafiri kutoka 88.5 Dar es salaam mpaka 104.4 Dodoma na kuziunganisha nguvu zao kwa ajili ya kuhakikisha wanakamilisha walichokianzisha….. yani kuizindua video yao ya wimbo wa miaka 50 (Tanzania @50) .
Kwenye rekodi za Tanzania, hii itakua mara ya kwanza kufanyika kwa tukio kubwa kama hili kutokana na level waliyoiweka, maandalizi, wageni waalikwa lakini pia njia ya maamuzi bora ya nguvu ya ushawishi kuwafikia Watanzania.
Kuanzia Diamond Platnumz, Mwasiti, Roma, Baba Level, Quick Rocka, Izzo B, Shilole, Mwana FA, Meninah, Linex, Mrisho Mpoto, Wema Sepetu na mastaa wengine mbalimbali watakutana na Watanzania wengine katika mkusanyiko usio na kiingilio Jamuhuri Stadium leo June 14 2014 saa nane mchana kuendelea kuusambaza upendo na uzalendo.
Unaambiwa haijawahi kutokea Vijana wa kizazi cha sasa kufanya tukio kama hili la kuwakusanya na kuwahamasisha Watanzania wengine kwa namna hii.
Pamona na hayo yote, hili tukio litafanyika mbele ya Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Znz Dk. Shein, Waziri mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine wa serikali akiwemo spika Anne Makinda.
Hili ni tukio ambalo litawafanya Watanzania kuwaona mastaa wao mbalimbali kwenye stage ambapo kama uko mbali na Dodoma, inabidi ukae karibu na TBC 1, Star TV na CloudsTV ambazo zitaonyesha kila kitu live mtu wangu.