Maandalizi ya kuaga miili ya vijana kumi wa JKT na askari mmoja wa JWTZ Pamoja na raia wawili waliofariki kwenye ajali ya basi la Kampuni ya Igunga Express June, 14 katika eneo la Igodima kata ya Mwansekwa jijini Mbeya, zoezi hili linafanyika kwenye viwanja vya Jeshi la kujenga Taifa 844 KJ Itende,
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika anaongoza Viongozi mbalimbali Maafisa wa majeshi mbalimbali ikiwemo JWTZ pamoja na wafiwa kuaga miili hiyo.