Leo July 20, 2017 Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Temeke na kusomewa makosa mawili ya kuendesha gari bila bima na kutotii amri ya Ofisa wa Polisi barabarani.
Akisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Josephat Mahugo mbele ya Hakimu Eliarusia Nassary, Mbunge Mtolea alidaiwa kutenda kosa la kuendesha gari lisilokuwa na bima July 19, 2017 maeneo ya Kurasini Dar es Salaam pia katika tarehe hiyo hiyo mshitakiwa alikaidi amri ya Ofisa wa Polisi ya kumtaka apeleke gari kituo cha Polisi, Kilwa Road.
Baada ya kusomewa makosa hayo, Mtolea alikiri makosa yote ambapo alisomewa maelezo ya awali (PH) kisha kuhukumiwa kulipa faini ya Pound 100 na Tsh. 30,000.
Katika hukumu yake, Hakimu Nassary alisema, kosa la kwanza mshtakiwa anatakiwa kulipa Pound 100 sawa na Tsh. 291,700 au kifungo cha miezi 6 jela wakati kosa la pili ni kulipa faini ya Tsh. 30,000 au kifungo cha miaka 2 jela ambapo baada ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi Hashim Mziray aliieleza kuwa mteja wake atalipa faini hiyo.
Kila kitu kipo kwenye hii video unaweza kutazama kwa kuplay!!!
Mabadiliko yaliyofanywa na TCU baada ya agizo la JPM kuhusu Udahili Elimu ya Juu…tazama kwenye VIDEO hii kila kitu!!!
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aligoma kutoka katika chumba cha Mahakama ya Wilaya Dodoma baada ya kufanya shughuli zake za uwakili kwa kuhofia kukamatwa na Polisi waliosemekana kumsubiri nje wamkamate kwa tuhuma za uchochezi…tazama kila kitu kwenye VIDEO hii!!!