Watu zaidi ya hamsini wanaoshutumiwa kwa “uchawi” wamefariki nchini Angola baada ya kulazimishwa kunywa mchanganyiko wa mitishamba ili kubaini kama wanafanya vitendo vinavyochukuliwa kuwa vya uchawi, kulingana na vyanzo vya ndani na polisi kwenye redio ya taifa siku ya Alhamisi.
Waangola wengi hukimbilia kwa “wachawi” waliopewa mamlaka ya juu zaidi kulingana na baadhi ya imani, kutatua mzozo au kabla ya kufanya uamuzi.
Madai ya uchawi mara nyingi hutatuliwa na waganga wa kienyeji, au “marabouts,” kwa kumfanya mtuhumiwa anywe kinywaji chenye sumu cha mitishamba kiitwacho “Mbulungo.” Kifo kinaaminika na wengi kuthibitisha hatia.
“Zaidi ya waathiriwa 50 walilazimishwa kunywa maji haya ya ajabu ambayo, kwa mujibu wa washauri wa jadi, yanathibitisha kwamba mtu huyo anafanya uchawi au la,” amesema Luzia Filemone, ofisa mteule wa manispaa ya Camacupa , kwenye redio ya taifa ambapo idadi ya vifo imeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
“Idadi ya vifo vilivyohusishwa na unywaji wa kioevu hiki iliongezeka kutoka 30 hadi 50,” mkuu wa polisi wa eneo hilo António Samba ameiambia redio ya taifa.
Hakuna sheria nchini Angola inayoadhibu rasmi “uchawi”. Lakini kiutendaji, “waze wa busara” wanaochukuwa nafasi ya washauri ndani ya baadhi ya jamii wanashauriwa ili kubaini kama mtu ni “mchawi”.
Vitendo hivi vinapingwa hasa na Kanisa katika koloni hili la zamani la Ureno lenye Wakatoliki wengi.
Wakati wa safari ya 2009 nchini Angola, Papa Benedict aliwataka Wakatoliki kuachana na ibada znazo husiana na uchawi.