Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amefika katika Soko la Mwenge ambalo limetekea kwa moto usiku wa kuamkia leo huku akisema Fedha nyingi zimeteketea baada ya kuonekena kwa vipande vya Fedha vya Shilingi Elfu Kumi.
Moto huo mkubwa umesababisha hasara kwa maduka zaidi ya 30 pamoja na Fedha kuunga na baadhi ya bidhaa kuharibika .
“Nimeona hali iliyotokea hapa kwa kweli nasikitika sana na tupo na watu wa Tanesco hapa nilikuwa najaribisha kidogo kuwauliza je itaweza kuwa ni hitilafu ya umeme wanasema Mkuu wa mkoa tupe muda kidogo, nimeuliza watu wa Fire wanasema tupe muda kidogo lakini kwa ujumla hasara iliyopatikana hapa haihitaji kwenda Chuo Kikuu kwenda kujifunza na kwa bahati mbaya sana inaonyesha Wafanyabiashara wengi hawajui thamani ya bei kwa sababu ndani ya moto huu kuna Pesa nyingi zimeungua ambazo inaonekana kuna vipande vya Elfu Kumi Kumi vingi vimesagaa vikiwa vimeungua,
Hivyo yafuatayo lazima yafanyike kwa haraka la kwanza kufahamu chanzo cha moto huu kwa haraka na kama kuna mtu amesababisha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,”.